Angalizo dhidi ya samaki Papa huko Australia

Samaki Papa ambao ni hatari katika fukwe huko Australia
Maelezo ya picha,

Samaki Papa ambao ni hatari katika fukwe huko Australia

Polisi magharibi wa Australia wamewataka watu kukaa mbali na maji maeneo ya fukwe kutokana na msichana mmoja kushambuliwa vibaya na samaki papa hapo jana.

Msichana huyo mwenye miaka 17 wakiwa na baba yake walikuwa maeneo hayo ya fukwe wakirambaza mitandaoni mida ya mchana katika maeneo ya ufukwe wa Wylie karibu na Esperance na ndipo binti huyo alishambuliwa kwa kung'atwa kwenye paja.

Ufukwe huo umefungwa kwa saa arobaini na nane na boti zinaendelea kufanya doria katika eneo hilo wakati mamlaka zikifanya uchunguzi kuhusiana na papa anayehusika na mkasa huo.

Shambulizi hilo limezua mjadala kuhusiana na kutumia vyandarua maalumu za kujikinda na mashambulizi ya smaki huyo.