Mimi ni mjamzito:Serena

Serena Williams amekiri kuwa na mimba
Image caption Serena Williams amekiri kuwa na mimba

Mchezaji wa tenisi nambari mbili kwa sasa duniani, Serena Williams amejitokeza katika mitandao ya kijamii na kuandika kuwa ni mjamzito.

Mwanadada huyo mwenye mika 35 aliweka picha yake kwenye snapchat akiwa amejipiga picha kwenye kioo na kuandika 20 weeks yaani majuma 20 kisha akaifuta hiyo post.

Iwapo itathibitika kwa hakika kuwa ni mjamzito, Serena anaweza kuzikosa Grans Slams tatu yaani French Open, Wimbledon na US Open.