Ugonjwa usiojulikana wawaua watu zaidi Liberia

Maafisa wamewashauri watu kuchukua tahadhari zilizochukuliwa wakati wa mlipuko wa Ebola ikiwemo kuosha mikono. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maafisa wamewashauri watu kuchukua tahadhari zilizochukuliwa wakati wa mlipuko wa Ebola ikiwemo kuosha mikono.

Watu wawili zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa usiojulikana ambao uliwaambukiza watu waliohudhuria mazishi mapema wiki hii katika kaunti ya Sinoe nchini Liberia kusini mashariki mwa mji mkuu Monrovia.

Vifo hivyo vinafikisha idadi ya watu waliofariki kuwa 11.

Watu watano kwa sasa wametengwa na wengine wanne wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kupata nafuu.

Mamlaka hata hivyo zinasema kuwa si mlipuko mwingine wa Ebola.

Uchunguzi bado haujaonyesha chanzo cha ugonjwa huo usiojulikana lakini wizara ya afya ina mpango wa kupeleka sampuli za damu katika mahabara za ngambo ikiwemo Marekani.

Maafisa wamewashauri watu kuchukua tahadhari zilizochukuliwa wakati wa mlipuko wa Ebola ikiwemo kuosha mikono.