Trump aadhimisha siku 100 kwa kuwashambulia wanahabari
Huwezi kusikiliza tena

Rais Trump wa Marekani aadhimisha siku 100 kwa kuwashambulia wanahabari

Rais wa Marekani Donald Trump ameadhimisha siku mia moja uongozini kwa kutoa hotuba ya kushambulia wanahabari na kutetea mafanikio yake.

Bwana Trump amewaaambia wafuasi wake huko Pennsylvania kwamba ameridhika kuwa pamoja nao badala ya kuhudhuria dhifa ya chakula cha jioni na wanahabari ama 'Correspondents diner' iliyokuwa ikifanyika katika ikulu ya White House wakati huo.