Mhalifu wa kivita raia wa Austria akamatwa Poland

Alikuwa miongoni mwa waliotafutwa kwa uhalifu wa kivita nchini Ukraine
Image caption Alikuwa miongoni mwa waliotafutwa kwa uhalifu wa kivita nchini Ukraine

Raia mmoja wa Austria amekamatwa nchini Poland kwa tuhuma za kufanya uhalifu wa kivita Mashariki mwa Ukraine wakati akiwa anapigana kwa ajili ya serikali ya Ukraine.

Waendesha mashtaka nchini Austria wanasema kuwa kijana huyo wa miaka 25 anatuhumiwa kwa kuwaua waasi ambao walipaswa kujisalimisha katika uwanja wa ndege wa Donetsk pamoja na wananchi wasiokuwa na hatia.

Alikamatwa Mashariki mwa nchi ya Poland katika mpaka wa Dorohusk akijaribu kuingia nchini Ukraine.