UEFA: Ajax yaifumua Lyon katika Europa Ligi

Klabu ya soka ya Ajax Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Klabu ya soka ya Ajax

Klabu ya soka ya Ajax ya Uholanzi imefanikiwa kuichapa Lyon ya Ufaransa bao 4-1 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Uefa Europa mchezo uliopigwa dimba la Amsterdam Arena.

Magoli ya Ajax yamefungwa na wachezaji Bertrand Traore mabao mawili, Kasper Dolberg, Amin Younes na huku bao la kufutia machozi la Lyon likifungwa na Mathieu Valbuena.

Mchezo wa kwanza mwingine wa Nusu fainali unapigwa leo Alhamisi ambapo Manchester United watakuwa ugenini dhidi ya Celta vigo vijana wa Eduardo Berizzo,na wakati huo huo imeripotiwa ya kwamba wachezaji waliokuwa wanakabiliwa na majeruhi wanne wa Manchester United Paul Pogba, Eric Bailly, Chris Smalling na Phil Jones watakuwepo katika mchezo huo.

Mada zinazohusiana