Juventus bingwa wa Seria A kwa msimu wa sita mfululizo

Juventus Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kocha wa Juventus Massimiliano Allegri, akishangilia na mchezaji wake Juan Cuadrado Juan

Vibibi vizee vya Turin Klabu ya Juventus imeweka historia ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya nchini Italia kwa mara ya sita mfululizo .

Juventus wametwaa ubingwa huo wa Seria A baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya vibonde wa ligi hiyo klabu ya Crotone.

Mabao ya ushindi ya Juve katika mchezo huo yalifungwa na mshambuliaji Mario Mandzukic katika dakika ya 12 ya mchezo , Paulo Dybala akaongeza bao la pili katika dakika ya 39, Mlinzi Alex Sandro akapiga msumari wa mwisho katika dakika ya 83.

Hili ni kombe la pili kwa timu hiyo baada ya wiki iliyopita kutwaa taji la Copa italia kwa kuichapa Lazio kwa mabao 2 -0.