Wanawake wajitosa katika kutibu mifugo Somalia
Huwezi kusikiliza tena

Wanawake Somalia wajitosa katika kazi ya kutibu mifugo

Ufugaji ni uti wa mgongo wa jamii ya kisomali na nchini Somalia. Wanyama hao hutegemewa kuzalisha mapato kwa familia nyingi. Lakini licha ya hayo, nafasi ya wanawake katika ufugaji umedunishwa kwa kuonekana viumbe wasio na nguvu. Hata hivyo, hali hiyo inaonekana kubadilika kwani ongezeko la madatari na wataalamu wa mifugo wa kike imewapaaisha wanawake na kuwafanya viungo muhimu katika uboreshaji wa hali yao. Mwandishi wetu Abdinoor Aden amezuru eneo la Puntland, Kaskazini mashariki mwa Somalia na kutuandalia ripoti ifuatayo.

Mada zinazohusiana