Marekani : Aliyemuoa mwalimu wake ataka mahakama iwatenganishe bila sababu

Mary kay Fualaau na Vili Fualaau Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Mary Kay Fualaau (kushoto) alitumikia kifungo cha jela kwa kufanya ngono na Vili Fualaau (kushoto) kabla ya kuoana mwaka 2005

Mwanamume amewasilisha kesi mahakamani akitaka atengane na mkewe ambaye ni mwalimu wake wa zamani aliyefungwa kwa kufanya nae ngono akiwa na umri wa miaka 12.

Vili Fualaau, ambaye sasa ana umri wa miaka 33, amewasilisha nyaraka za kesi kwenye mahakama ya jimbo la Washingto, Marekani , akitaka ndoa yake ya miaka 12 na Bi Mary Kay Fualaau (zamani akijulikana kama Letourneau), mwenye umri wa miaka 55 ivunjwe.

Bi Fualaau aliolewa akiwa na umri wa miaka 34- akiwa na watoto wanne alipoanza uhusiano wa kindoa na Vili Fualaau.

Baada ya kutumikia kufungo cha jela , wawili hao walioana kwa siri mnamo mwaka 2005.

Bwana Fualaau aliwasilisha kesi ya kuachana nae mapema mwezi huu bila kuelezea sababu ya uamuzi wake huo, ilibainika.

Katika ombi lake kwa mahakama , aliandika kwamba iwe yeye wala mkewe hakuna aliye na mali wala mkopo, vimeripoti vyombo vya habari vya marekani.

Bwana Fualaau, ambaye ana watoto wawili na mkewe , pia alisema kwa sasa hawamtegemei tena, akiomba wawili hao wagawanywe kile walichoweza kutafuta pamoja kwa haki.

Mkewe hajatoa kauli yoyote kwa umma juu ya uamuzi wa mumewe.

Bwana Fualaau alikuwa darasa la sita alipoanza uhusiano wa kimapenzi mjini Seattle mwaka 1996.

Akiwa mwalimu Bi Fualaau alikamatwa mwaka 1997 alipokuwa na mimba ya mtoto wao wa kwanza ,na baadaye alikiri kufanya kosa la ubakaji wa mtoto.

Huku yake ya kwanza ya miezi sita ilipunguzwa baadae na kuwa ya miezi mitatu chini ya misingi kwamba angelikosa mawasiliano na mwanafunzi wake wa zamani.

Lakini katika kipindi cha wiki kadhaa wawili hao walikamatwa wakifanya ngono, na akafungwa miaka saba.

Alipata mtoto wao wa pili.