Watoto 15 wamefariki Sudan Kusini

Raia wa Sudan Kusini wakimbia Vita vya wenyewe kwa wenyewe
Image caption Raia wa Sudan Kusini wakimbia Vita vya wenyewe kwa wenyewe

Serikali ya Sudan Kusini, inasema kuwa yamkini watoto 15 wamefariki, kutokana na kile kinachosemwa makosa katika jaribio la kuwapa chanjo cha ugonjwa wa ukambi.

Wahudumu wa afya katika jimbo la Eastern Equatoria, mara kwa mara wamekuwa wakitumia sindano moja chafu kuwapa chanjo watoto wengi.

Waziri wa Afya wa Sudan Kusini, Riek Gai Kok, amesema kuwa timu inayohusika katika kampeini hiyo ya kuwapa watoto chanjo, hawajasoma au kupata mafunzo yoyote ya kiafya.

Huduma za kiafya nchini Sudan Kusini zimelemaa kabisa tangu kuanza upya kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013.