Madaktari wapendekeza vifaa vya kutibu maradhi ya moyo kwenye ndege

AED ni kifaa kinachoweza kubebwa kwwa urahisi, ambacho hutumika kuchunguza mpigo wa moyo na kinatuma ujumbe hadi kwwa moyo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

AED ni kifaa kinachoweza kubebwa kwwa urahisi, ambacho hutumika kuchunguza mpigo wa moyo na kinatuma ujumbe hadi kwwa moyo

Mashirika yote ya ndege duniani yanatakiwa kuweka mitambo ya kimatibabu ya kushughulikia matatizo ya mayo hasa katika hali ya dharura, hayo yamesemwa na madaktari.

Hali kama hiyo ni adimu sana lakini inaashiria taarifa ya vifo vingi ndani ya ndege, takwimu zinaonyesha.

Jopo kazi lililobuniwa kupigia msasa taarifa hiyo, inasema kwamba, electrocardiograms (ECGs), yaani kifaa kinachotumiwa kupima mpigo wa moyo usiku kucha na defibrillators, mtambo mdogo unaotumiwa kudhibiti mtetemeko wa moyo ambao unaweza kusababisha damu kuganda, kupatwa na ugonjwa wa

kiharusi au kusimama ghafla kwa moyo na kwwa ujumla mitambo ambayo inashughulikia matatizo yote ya moyo.

Zinafaa kuwekwa ndani ya ndege.

Karibu watu 1,000 kila mwaka wanapatwa na mshtuko wa moyo angani; hayo ni kwwa mjibu wa takwimu zilizotolewa katika mkutano wa afya unaofanyika huko Geneva.

Hata inagawa mshutuko wa moyo unachangia asilimia 1% ya matatizo ya dharura ya kimatibabu ndani ya ndege, yanaweza kuwa na hatari kubwa mno.

Madaktari hao walkiongozwa na Prof Jochen Hinkelbein wa Chuo Kikuu cha Cologne, Ujerumani na Rais wa German Society for Aerospace Medicine, wamebuni mapendekezo ya mshutuko wa moyo kwenye safari za ndege.