Kuna hofu abiria wote 120 waliokuwa kwenye ndege ya Burma, wamefariki

Ndege ya Mizigo iliyopotea ikiwa na watu 120 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndege ya Mizigo iliyopotea ikiwa na watu 120

Matumaini yanazidi kufifia kwa abiria wote 120, ambao walikuwa ndani ya ndege moja ya jeshi la Burma, iliyopotea angani ilipokuwa ikipaa katika maeneo ya bahari ya Andaman.

Duru zinasema kuwa, kulikuwa na wanajeshi 106, familia zao na wahudumu 14 wa ndege wakati wa kupotea kwa ndege hiyo.

Ndege hiyo muundo wa Y8 ya mzigo iliyoundiwa China, ilikuwa imemaliza muda wa nusu saa tangu ilipopaa angani kutoka uwanjani.

Ndege ya Burma iliyo na abiria 100 yatoweka

Facebook kuwa somo chuo kikuu India

Myanmar inachunguza 'utumwa wa watoto'

Taaarifa za hivi punde zasema kuwa, mabaki ya ndege imeonekana baharini, huku ndege za kijeshi zikiwemo helikopta, zikiendelea kusaka eneo hilo, ili kuokoa manusura.

Hayo ni kwa mjibu wa taarifa kutoka kwa wakuu wa nchi hiyo.

Ndege hiyo ya kijeshi, ilikuwa ikipaa kati ya Yangon (Rangoon) na mji ulioko kusini mwa nchi hiyo wa Myeik.

Shughuli za kutafuta na kuokoa manusura zinaendelea.

Image caption Ramani ya Myanmar ama Burma

"Tulipoteza mawasiliano na ndege hiyo mwendo wa saa nne na dakika 35 leo asubuhi saa za Afrika Mashariki [07:05 GMT], pale ndege hiyo ilipofika maili 20 magharibi mwa mji wa Dawei," jeshi la Burma limesema kwa njia ya taarifa.

Awali shirika la habari la AFP lilisema kuwa kulikuwa na abiria 105 na wafanyikazi 11 kwenye ndege hiyo.

Ndege za wanajeshi pamoja na helikopta zimetumwa katika eneo hilo katika shughuli za kuwatafuta manusura au mabaki ya ndege hiyo ambayo kufikia sasa inaaminika kuwa imeanguka.

Taarifa inaongeza kuwa, ndege hiyo ilikuwa angani ikivuka bahari ya Andaman, pale ilipotoweka.