Waasi wa Farc nchini Colombia wasalimisha asilimia 30% ya silaha

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Waasi wa wameahidi kurejesha silaha zao zote ifikiapo Juni 20

Waasi wa kundi la Farc nchini Colombia, wanasema kuwa wamesalimisha asilimia 30% ya silaha kwa wachunguzi wa shirika la Umoja wa mataifa (UN), chinia ya maafikiano ya amani.

Watawasilisha tena silaha zipatazo thuluthi moja ifikiapo Jumatano ya wiki ijayo, huku itakayosalia itawasilishwa katika muda wa mwezi mmoja ujao.

Silaha hizo zitahifadhiwa katika maeneo tofauti 26 kote nchini humo.

Waasi wa FARC kusitisha mapigano

Kiongozi wa waasi wa FARC arejea Colombia

Colombia yaidhinisha sheria ya msamaha.

Baada ya nusu karne ya mapigano na miaka kadhaa ya mazungumzo ya kukomesha vita, serikali na kundi hilo kubwa la waasi nchini humo, zilitia saini ya kusitisha vita mwaka jana.

Kuna bunduki na bastola 7,000, ambazo zinafaa kuwasilishwa kabla ya kundi hilo la Farc - Revolutionary Armed Forces of Colombia - kugeuka na kuwa chama cha kisiasa.

Image caption Waasi wa Farc wakijumuisha wapiganaji wa kike

Kinara mkuu wa Farc Rodrigo LondoƱo Echeverri, ambaye anafahamika kwa jina maarufu Timochenko, siku ya Jumatano alitangaza kwenye mtandao wake wa kijamii wa tweeter kuwa, wapiganaji wake watawasilisha silaha bila matatizo yoyote.

Duru kutoka kwa serikali na Umoja wa Mataifa, zinathibitisha kuwa silaha zimewasilishwa.

Waasi hao wa Farc wako na muda hadi Juni 20 kuwasilisha silaha zote walizonazo- makataa iliyoongezwa tangu Mei 30.