Mapigano yaua kadhaa Afrika ya Kati

Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa, akilinda usalama Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa, akilinda usalama

Watoa misaada ya kibinaadamu wamearifu kwamba watu arobaini wameuawa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, siku moja baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya upande wa serikali na vikundi vya waasi nchini humo.

Mapigano makubwa yaliibuka katika mji wa Bria, ulioko upande wa kaskazini mwa mji mkuu, Bangui mapema wiki hii.

Mji huo uko chini ya usimamizi wa meya , Maurice Belikoussou, alisikika akizungumzia juu ya maiti za watu zilizotapakaa katika mitaa mbalimbali.

Makubaliano ya suluhu yaliwekwa saini mjini Roma, Italia yakijumuisha usitishwaji mapema wa mapigano, yakiwa na lengo la kufikia mwisho wa mapigano yaliyodumu miaka kadhaa yakihusisha vurugu kati ya wanamgambo wa Kikristo na Waislam.