Maporomoko ya ardhi yauwa 15 China 100 hawajulikani waliko

Wahudumu wa matibabu wakiendelea kuwasaka manusura Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahudumu wa matibabu wakiendelea kuwasaka manusura

Juhudi zinaendelea za kuwapata manusura wa janga baya la maporomoko ya ardhi katika jimbo la Sichuan nchini China.

Kufikia sasa maiti 15 ya wahasiriwa wa janga hilo la kimaumbile, zimepatikana katika maporomoko hayo ya ardhi katika kijiji cha Xin-mo.

Zaidi ya watu 100 hawajulikani waliko, huku wataalamu walionukuliwa na runinga ya nchi hiyo, wakisema matumaini ya kuwapata wakiwa hai ni finyu mno.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Zaidi ya watu 100 hawajulikani waliko

Runinga ya shirika la Xinhua, imetangaza kuwa zaidi ya wafanyikazi 3,000 wa huduma za dharura, wamefika katika kijiji cha maeneo hayo ya milima milima, ambayo hutembelewa sana na watalii, ili kujaribu kuwaokoa waathiriwa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahudumu wa majanga ya dharura wanasaka maporomoko hayo ili kujaribu kuwapata manusura

Wanatumia matinga tinga, vifaa vya kielektroniki na mbwa wa kunusia, ili kubaini maisha ya watu ambao wamenaswa ndani ya maporomoko hayo.