Rais Assad ahudhuria ghafla sala za Eid mjini Hama

Rais Assad
Image caption Rais Assad

Rais wa Syria, Bashar al-Assad, amefanya ziara ya ghafla isiyotarajiwa nje ya mji mkuu wa nchi hiyo Damascus, alikohudhuria maombi ya Eid, katika mji wa Hama, zaidi ya kilomita 200 kaskazini mwa nchi hiyo.

Ni sehemu ya mbali zaidi kuwahi kusafiri, ndani ya Syria, tangu mapigano yalipoanza nchini humo miaka 6 iliyopita.

Runinga ya nchi hiyo, ilipeperusha picha ya Rais Assad, akisali ndani ya msikiti mmoja mkubwa mjini Hama nyumba ya imamu wa msikiti huo, ndani ya umati mkubwa wa waumini wengine.

Ziara hiyo ya Assad inatukia wakati ambapo wanajeshi wa serikali yake, wakiungwa mkono na ndege za kijeshi za Urusi, wakiendelea kupata nguvu dhidi ya makundi ya waasi.