Mashua yazama Colombia 6 wafa maji, 16 hawajulikani waliko

Msako na shughuli za uokozi zinaendelea Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGES
Image caption Msako na shughuli za uokozi zinaendelea

Idara ya polisi nchini Colombia, imesema kuwa yamkini watu 6 wamefariki ika ajali ya kuzama kwa boti moja la abiria katika bwawa moja, katika mji mmoja ulioko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Watu 16 hawajulikani waliko, baada chombo cha ghorofa nne, lilipoanza kujaa maji mara tu lilipo n`goa nanga katika ziwa moja la kujiundia, karibu na mkahawa mmoja maarufu kwa watalii la Guatapé, kilomita 45 mashariki mwa Medelini, siku ya Jumapili.

Kulikuwa na watu 150 ndani ya chombo hicho.

Kwa mjibu wa mtu mmoja aliyeshuhudia ajali hiyo, Juan Quiroz, ameiambia BBC kuwa, chombo hicho kilichukua chini ya dakika 5 kuzama.

Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGES
Image caption Walio okolewa wam,etamaushwa na ajali hiyo

Maboti mengine madogo madogo yalifika kwa kasi na kuanza kuwaokoa watu kutoka majini na orofa ya juu ya chombo hicho.

Aidha, ndege za helikopta na wapiga mbizi wa kijeshi wameonekana mahali pa mkasa huo wakijaribu kuwaokoa manusura.

Hakujatolewa taarifa zaidi ya kilichosababisha chombo hicho cha majini kuzama.

"Hali inaonekana kuwa mbaya zaidi," afisa mmoja wa serikali katika eneo hilo amewaambia wanahabari.

Zaidi ya watu 20 wamekimbizwa hospitalini katika mji wa Guatapé.

Image caption Ramani inayoonyesha mji wa Guatape

Luis Bernardo Morales, kapteni mmoja wa idara ya zima moto ambaye anahusika moja kwa moja katika shughuli za uokoaji, amesema kuwa boti hilo lilikuwa karibu na bandari pale lilipozama.

"Hatujafahamu kama kiini cha ajali hiyo ilikuwa ni matatizo ya kimitambo, ubeba watu kupita kiasi au mawimbi ziwani," Shirika la habari la AFP lilimnukuu akisema.

Guatapé ni eneo maarufu kwa watalii katika mji wa Andean, unaojulikana kwa michezo mingi ya majini na sehemu ya burudani.

Mada zinazohusiana