Jacob Zuma na makamu wake walazimishwa kusalimiana

Jacob Zuma na makamu wake walazimishwa kusalimiana
Maelezo ya picha,

Jacob Zuma na makamu wake walazimishwa kusalimiana

Aliyekuwa mke wa rias wa kwanza wa Afrika Kusini Nelson Mandela,

Winnie Madikizela Mandela aliwalazimisha viongozi wawili maaruf nchini humo rais Jacob Zuma na makamu wa rais Cyril Ramaphosa kusalimiana.

Wawili hao walikuwa katika mkutano wa chama cha ANC mjini Johannesburg.

Bwana Ramaphosa anataka kumrithi rais Zuma na amekuwa akimkashifu rais huyo kwa uhusiano wake na familia ya Gupta.

Maelezo ya picha,

Rais Jacob Zuma na makamu wake Cyril Ramaphosa

Mojawapo ya mambo yaliobanikika katika barua pepe zilizotajwa kuwa 'Guptaleaks', ni kwamba rais Zuma alikuwa amepanga kwenda kuishi katika miliki za Kiarabu UAE.

Madai ambayo yamekanwa.

Mengine yalionyesha kuwa familia hiyo ya Gupta imekuwa na ushawishi mkubwa serikalini.