Usher Raymond azuru mbuga ya Serengeti Tanzania

Usher Raymond akipiga picha na familia yake katika mbuga ya Serengheti nchini Tanzania Haki miliki ya picha Picha kwa niaba ya mtandao wa Twitter
Image caption Usher Raymond akipiga picha na familia yake katika mbuga ya Serengheti nchini Tanzania

Msanii wa Marekani Usher Raymond yuko ziarani nchini Tanzania akitembelea eneo la uhifadhi wa wanyama pori la Serengti National Park.

Bwana Raymond alichapisha baadhi ya picha akiwa na familia yake katika akaunti yake ya Twitter.

Alielezea hali ilivyo katika eneo hilo kama ya kufurahisha .

Ripoti za Usher Raymond kuzuru Tanzania zilisambaa kwa haraka nchini humo.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Usher Raymond

Watu wengine maarufu akiwemo mchezaji wa zamani wa Manchester United na Real Madrid David Becham, aliyekuwa mchezaji wa Liverpool Mamadou Sakho, mchezaji wa Everton Morgan Schneiderlin ni miongoni mwa wale waliozuri katika sehemu mbali mbali za kitalii nchini humo mwaka huu.

Vivutio vya kitalii nchini Tanzania kama vile mbunga ya uhifadhi wa wanyama pori ya Serengeti na mlima Kilimanjaro ni vivutio vinavyoongoza kwa utalii ambapo watu wengi maarufu wametembela.