Pakistan yashambulia IS

wanajeshi wakilinda usalama Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption wanajeshi wakilinda usalama

Wanajeshi wa Pakistan wameanzisha operesheni kubwa ya kijeshi dhidi ya wapiganaji wa Islamic State katika mkoa wa kaskazini Magharibi, ulio karibu na mpaka wa Afghan.

Msemaji wa Jeshi la nchi hiyo amesema kwamba wapiganaji hao wenye itikadi kali wamejiimarisha ndani ya Afghanistan na hivyo wanapaswa kuzuiwa kufanya hivyo ndani ya Pakistan.

Operesheni hiyo inalenga zaidi kufanywa katika mkoa wa mpakani, huku ikiungwa mkono na jeshi la Anga la Pakistan.

Serikali ya nchi hiyo imekuwa ikikanusha uwepo wa kundi hilo la IS ndani ya nchi, licha ya mfululizo wa mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na kundi hilo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.