Al-Shabab wadai kuwaua wanajeshi 39 wa AU

Al-Shabab wadai kuwaua wanajeshi 39 wa AU Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Al-Shabab wadai kuwaua wanajeshi 39 wa AU

Kundi la wanamgambo wa al-Shabab nchini Somalia linasema kuwa limewaua wanajeshi 39 wa Muungano wa Afrika (AU) wakati walivizia msafara wao eneo la Lower Shabelle.

Hata hivyo AU haikutoa idadi ya wanajeshi waliouawa lakini iliandika katika mtandao wake wa Twitter kuwa uharibifu mkubwa ulifanywa kwa adui na wanajeshii wake nao waliuawa.

Al-Shabab washambulia kikosi cha AU Somalia

Vikosi vya Marekani vyaharibu ngome ya Al-Shabaab Somalia

Shambulio lawaua watu 6 Mogadishu

Naibu gavana wa eneo la Lower Shabelle Ali Nur, aliliambia shirika la Reuters kuwa wanajeshi 23 wa AU na mmoja wa Somalia waliuawa wakati wa kisa hicho cha siku ya Jumapili.