Ubelgiji ilifahamu kuhusu mayai yaliyoharibika

Mayai yaliyo na sumu ya kuuwa wadudu yakiharibiwa shambani nchini Uholanzi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mayai yaliyo na sumu ya kuuwa wadudu yakiharibiwa shambani nchini Uholanzi

Maafisa wakuu nchini Ubelgiji wamekiri kuwa, mnamo mwezi Juni, walifahamu mayai kutoka Uholanzi, huenda yalikuwa yameharibiwa na dawa ya kuuwa wadudu.

Msemaji wa mamlaka kuu ya usalama wa chakula nchini Ubelgiji Katrien Stragier, amesema kuwa waliweka siri kwa sababu ya uchunguzi kuhusu udanganyifu, kwamba mayai hayo yalikuwa na uwezekano wa kuingiliwa na dawa aina ya Fipronil.

Maduka makubwa ya jumla nchini Ubelgiji, Uholanzi na Ujerumani, yameondoa kabisa madukani bidhaa hiyo ya mayai.