Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 12.08.2017 na Salim Kikeke

Barcelona wanamgeukia sasa kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, 25, kwa sababu Liverpool wamegoma kabisa kumuuza Philippe Coutinho, 25. (independent)

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha,

Barcelona wanamgeukia sasa kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, 25, kwa sababu Liverpool wamegoma kabisa kumuuza Philippe Coutinho, 25. (independent)

Barcelona wanamgeukia sasa kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, 25, kwa sababu Liverpool wamegoma kabisa kumuuza Philippe Coutinho, 25. (independent)

Liverpool waliwaambia Barcelona wiki hii kuwa Philippe Coutinho, 25, bei yake ni pauni milioni 136.5. (Daily Record)

Barcelona bado wanamtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, 20, na watarejea na dau la pauni milioni 127. (AS)

Iwapo Barcelona watashindwa kumsajili Ousmane Dembele au Philippe Coutinho, wataamua kumfuatilia Ivan Perisic wa Inter Milan ambaye ananyatiwa na Manchester United. (Sport Italia)

Kiungo wa PSG Angel Di Maria, 29, huenda akachukuliwa na Barcelona kuziba pengo la Neymar. (Sport)

Maelezo ya picha,

Angelo Di Maria

PSG wamempa Kylian Mbappe mshahara wa pauni milioni 16.4 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka mitano ili kumshawishi kuondoka Monaco. (L'Equipe)

Kylian Mbappe, 18, anataka kuhamia PSG lakini hakuna mkataba wowote uliofikiwa na uhamisho huo huenda ukafanyika msimu ujao. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Eden Hazard

Real Madrid wameacha kumfuatilia Kylian Mbappe na huenda wakaamua kumfuatilia kiungo mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26. (Don Balon)

Chelsea bado hawajarejea na dau lililoongezeka kumtaka kiungo wa Leicester Danny Drinkwater, 27, baada ya Leicester kukataa dau la pauni milioni 15. (telegraph)

Tottenham wanazungumza na Ajax kutaka kumsajili beki wa kati Davinson Sanchez, 21, kwa pauni milioni 35. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiungo wa Real Madrid Isco

Kiungo wa Real Madrid Isco, 25, amesaini mkataba mpya wa miaka minne ambao una kifungu cha kutengua uhamisho cha pauni milioni 637. (AS)

Real Madrid wameacha kuwafuatilia Thibault Courtois, 25, wa Chelsea na David De Gea, 26, wa Manchester United. (Don Balon)

Manchester United wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Oliveirense, ya Ureno, Bruno Amorim, 19. (Noticias ao Minuto)

Maelezo ya picha,

Manchester United hawatalipa zaidi ya pauni milioni 90 kumsajili Gareth Bale kutoka Real Madrid. (Dario Gol)

Manchester United hawatalipa zaidi ya pauni milioni 90 kumsajili Gareth Bale kutoka Real Madrid. (Dario Gol)

Tukutane baadaye katika BBC Ulimwengu wa Soka ambapo tutakutangazia mechi ya Chelsea v Burnley.

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa.

Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumamosi njema.