Mark Zuckerberg amwambia bintiye kucheza nje

Picha ya familia ya Bwana na Bi Zuckerberg Haki miliki ya picha MARK ZUCKERBERG
Image caption Picha ya familia ya Bwana na Bi Zuckerberg

Muanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, tajiri Mark Zuckerberg, amemsihi bintiye mdogo kucheza nje na kufurahia maajabu ya kuwa mtoto, katika barua yenye hisia iliyochapishwa katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii.

Barua hiyo ilichapishwa siku ya Jumatatu alipotangaza kuzaliwa kwa mwanawe wa pili aitwaye August, na mkewe Priscilla Chan.

Katika barua ya kina waliyoiandika, wazazi hao wawili walizungumzia kuhusu maajabu ya kuwa mtoto na umuhimu wa kucheza.

Wawili hao waliweka mtandaoni barua kama hiyo kwa binti yao Max mnamo mwaka 2015.

Maaandishi hayo ambayo inaambatana na picha ya familia katika ukurasa wa Facebook wa Bwana Zuckerberg, kumhimiza mgeni huyo mchanga wala sio "kukua mkubwa haraka".