Nyama ya Punda yasababisha 'bei kupanda' nchini Kenya

Punda
Image caption Punda

Shirika moja linalohusika na maslahi ya wanyama nchini Kenya, linasema bei ya Punda imepanda mara dufu nchini humo kwa sababu ya nyama ya mnyama huyo kuongezeka hasa katika taifa la china taifa ambalo hununua kwa wingi bidhaa ya mnyama huyo

Kwa mujibu wa shirika hilo, sababu ya bei ya Punda kupanda kwa karibu asilimia 200 ni kutokana na ongezeka la biashara ya bidhaa za mnyama huyo huko Uchina ambako nyama ya punda ni kitoweo kilicho na walaji wengi.

Awali kichinjio cha punda kimoja tu kilikuwa kimefunguliwa nchini Kenya kwa minajili ya kusindika nyama ya punda na kisha kuuzwa huko Uchina.

Lakini sasa vichinjio vingine viwili vimefunguliwa kujaribu kukabiliana na mahitaji hayo yaliyoongezeka.

Image caption Punda ni mnyama wa kubeba mizigo na kufanya kazi ya sulubu, lakini nyama yake sasa imekuwa kitoweo

Mataifa kadhaa ya kiafrika yamepiga marufuku uuzaji ya nyama na bidhaa nyenginezo za punda, kwa ajili ya soko hilo la Uchina, kwa sababu punda ambao hutumiwa zaidi kwa ajili ya kusaidia kubeba mizigo mashambani, sasa idadi yao inapungua kwa kasi mno.

Kuna hofu kuwa huenda baadhi ya watu wanawasafirisha punda kimagendo hadi vichinjioni kutokana na kupanda kwa bei hiyo ya punda.

Gazeti moja la mashinani kwa jina Baringo News, inayosomwa katika maeneo ya Baringo na Nakuru katika bonde la Ufa nchini humo, na lililo karibu na kichinjio kikubwa zaidi cha punda Afrika Mashariki, inaripoti kuwa, kichinjia hicho kinafanya kazi huku kikipokea punda wengi mno wanaochinjwa na nyama yao kusafirishwa hadi nchini China.

Mataifa mengi yamepiga marufuku uchinjaji wa nyama ya punda yakiwemo mataifa kadhaa ya Afrika kama vile Uganda, Tanzania, Botswana, Niger, Burkina Faso, Mali, na Senegal.

Mataifa hayo aidha imeipiga marufuku China kunua ngozi ya punda kwani huenda ikaamiza kabisa wanyama hao duniani.

Soko kubwa la ngozi ya punda pia imeongezeka nchini Afrika Kusini.