Mwanawe Rais Jacob Zuma, Duduzane amekanusha madai ya ufisadi

Duduzane Zuma ni mmojawepo wa watoto 21 wa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini Haki miliki ya picha AFP
Image caption Duduzane Zuma ni mmojawepo wa watoto 21 wa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini

Mwanawe Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, amekanusha madai kuwa amehusika katika kashfa ya ufisadi.

na kuwa na uhusiano na mfanyibiashara mmoja mwenye utata.

Duduzane Zuma ameiambia BBC kuwa, hakuna "ambacho hakijasemwa" kuhusiana na mshirika wake wa kibiashara na familia ya Gupta.

Barua pepe ambayo inahusiana na familia ya Bwana Zuma na ile ya magupta na kuanzisha uchunguzi ambayo itaonyesha uwezekano wa kuingiliwa kisiasa.

Rais Zuma na familia ya Magupta, mara kwa mara yamekanusha kuhusika na jambo lolote baya.

Katika mahojiano ya kipekee yaliyofanywa na mwaandishi wa BBC Milton Nkosi, Duduzane Zuma amesema kuwa, uhusiano wake na familia tajiri ya Magupta, hauna mambo mengine zaidi kwani yeye ni "mtu mzuri anayependwa na wengi".

"Siamini kuna kitu wanachohitaji kutoka kwangu," alisema huku akiongeza kuwa: "Wananipenda. Na mimi pia nawapenda."

Duduzane Zuma, ambaye ni mmojawepo wa watoto 21 wa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, anasisiiza kuwa "si mfisadi".

"Binafsi sijawahi husika na biashara yoyote ya ufisadi," amesema.