Hali ya mbunge Tundu Lissu baada ya kushambuliwa kwa risasi Dodoma wiki iliyopita

Hali ya kiongozi wa upinzani wa Tanzania Tundu Lissu inatiliwa shaka baada kuibuka taarifa za kutatanisha kuhusiana na afya ya kiogozi huyo.

Bwana Lissu anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini kenya, baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana mjini Dodoma wiki iliyopita.

Mwandishi wa BBC Ambia Hisri alizunguma na Mchungaji Peter Msigwa-mbunge Iringa mjini na Godbless Lema-Mbunge wa Arusha Mjini, kutaka kufahamu zaidi hali ya Bw. Lissu