Wanawake waislamu nchini Tunisia waruhusiwa kuolewa na wanaume wasio waislamu

Tangazo hilo linakuja mwezi mmoja baada ya Rais Beji Caid Essebsi, kutoa wito kwa serikali kuondoa marufuku hiyo ya mwaka 1973.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Tangazo hilo linakuja mwezi mmoja baada ya Rais Beji Caid Essebsi, kutoa wito kwa serikali kuondoa marufuku hiyo ya mwaka 1973.

Rais wa Tunisia ametanga kuwa wanawake sasa wako huru kuolewa na wanaume wasio waislamu, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP

Tangazo hilo linakuja mwezi mmoja baada ya Rais Beji Caid Essebsi, kutoa wito kwa serikali kuondoa marufuku hiyo ya mwaka 1973.

Hadi sasa mwanamume ambaye si muislamu anayetaka kumuoa mwanamke wa Tunisia, alihitaji kubadili dini na kuwa muislamu na kutoa cheti cha kuonyesha kuwa amefanya hivyo.

Makundi ya kutetea haki za binadamu nchini Tunisia yamekuwa yakifanya kampeni ya kutaka kuondolewa marufuku hiyo wakisema kuwa inakiuka haki za binadamu za kumchagua mke au mume.

Tunisia inaonekana kuwa iliyopiga hatua mbele ya mataifa mengine katika masuala ya haki za wanawake, lakini bado kuna ubaguzi katika masuala ya urithi.