Wakuu wa jeshi Somalia wakiwemo waziri wa ulinzi wajiuzulu

Waziri wa ulinzi Abdirashid Abdullahi Mohammed alijiuzulu katika mkutano wa baraza la mawaziri Haki miliki ya picha SONNA
Image caption Waziri wa ulinzi Abdirashid Abdullahi Mohammed alijiuzulu katika mkutano wa baraza la mawaziri

Maafisa wakuu katika jeshi la Somalia wakiwemo mkuu wa jeshi na waziri wa ulinzi wamejiuzulu.

Kwa mujibu wa taarifa za serikali, waziri wa ulinzi aliamua kujiuzulu wakati wa mkutano wa wiki wa baraza la mawaziri.

Katika tukio jingine Mkuu wa Jeshi Ahmed Jimale Irfiid naye alijiuzulu hapo jana mchana.

Rais Farmajo hapo hapo akamteua Meja Jenerali Abdiweli Jama Gorod kuwa mkuu wa majeshi.

Hatua hiyo imekuja wakati ambao Somalia inakabiliwa na tishio la usalama kutoka kwa kundi la wapiganaji wa Al Shabab.

Nafasi ya Jenerali Mohamed Jima'le Irfid imechukuliwa na Jeneral Abdiweli Jama Hussein Gorod. Somalia kwa muda mrefu imekuwa ikikabiliwa na mashambulio kutoka kwa wapiganaji wa Al Shabab.

Mada zinazohusiana