Dada yake Raila Odinga kukamatwa kwa uchochezi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ruth Odinga

Dada wa kinara wa upinzani nchini Kenya Raia Odinga, atashtakiwa kwa kuchochea ghasia baada ya kushambuliwa kwa wafanyakazi wa tume ya uchaguzi IEBC wiki iliyopita, kwa mujibu wa mwendesha mkuu wa mashtaka nchini Kenya.

Ruth Odinga alikuwa ni naibu gavana wa kaunti ya Kisumu.

Mwendesha mashtaka mkuu nchini Kenya Keriakor Tobiko aliamrisha Ruth Odinga akamatwe.

Bw. Odinga alikuwa anawania urais pamoja na Rais Uhuru Kenyatta kwenye marudio ya uchaguzi wa urais siku la Alhamisi, lakini aljiondoa mapema mwezi huu, akisema kuwa uchaguzi huo hautakuwa wa huru na haki.