Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 27.10.2017

Chelsea inajiandaa kumrudisha mkufunzi wake wa zamani Carlo Ancelotti ambaye atachukua mahala pake Antonio Conte. (Sun)
Image caption Chelsea inajiandaa kumrudisha mkufunzi wake wa zamani Carlo Ancelotti ambaye atachukua mahala pake Antonio Conte. (Sun)

Chelsea inajiandaa kumrudisha mkufunzi wake wa zamani Carlo Ancelotti ambaye atachukua mahala pake Antonio Conte. (Sun)

Arsenal itamuuza mshambuliaji wake Alexis Sanchez kwa dau lisilipungua £30m kwa Manchester, 28, mnamo mwezi Januari. (Mirror)

The Gunners wako katika mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Stuttgart ambaye ni raia wa Uturuki Berkay Ozcan, 19. (BeinSports - in Turkish)

Image caption Hatma ya Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger kujulikana baada ya kukamilika kwa msimu huu

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger, ambaye ana kandarasi ya mwaka mmoja ataketi chini mwisho wa msimu huu kutathmini ukufunzi wake na bodi ya klabu hiyo. (Express)

Mkufunzi wa Watford Marco Silva, ambaye anapigiwa upato kuiongoza Everton amesema kuwa haondoki Watford. (Mirror)

Liverpool na Newcastle zinajiandaa kumsajii kipa wa klabu ya Porto ,36 Iker Casillas. (Sun)

Image caption Phillipe Coutinho

Liverpool inataka Yuro 150m kumuuza mchezaji anayesakwa na Barcelona Philippe Coutinho - ikiwa ni Yuro 50m chini ya dau walilotaka kulipwa baada ya mchezaji huyo wa Brazil kutaka kununuliwa msimu ulioipita (Mundo Deportivo - in Spanish)

Liverpool itampatia kinda wa Uingereza anayechezea timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 Rhian Brewster, ambaye alifunga hat-trick mbili katika kombe la dunia , kandarasi nzuri wakati atakapofikisha umri wa miaka 18. (Daily Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Etienne Capoue, 29

Kiungo wa kati wa Watford Etienne Capoue, 29, anataka kuandikisha mkataba wa muda mrefu na klabu hiyo.(Evening Standard)

Klabu ya Uhispania Sevilla inajiandaa kuwasilisha ombi la kumnunua mshambualiji wa klabu ya Monaco raia wa Montenegro Stevan Jovetic, ambaye analengwa na klabu ya Brighton. (Talksport)

Manchester United, Arsenal na Bayern Munich zinamchunguza mshambuliaji wa Barcelona Jose Arnaiz, 22. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwekezaji wa Dubai Amanda Staveley

Wamiliki wa Liverpool's walikataa makubaliano yenye thamani ya hadi £1.5bn kuiuza klabu hiyo kwa wawekezaji wanaoongozwa na mwekezaji wa Dubai Amanda Staveley. (The National)

Barcelona huenda ikabadilisha jina la uwanja wake na kuwa Nou Camp Grifols kuanzia msimu ujao.

Klabu hiyo inakaribia kutia kandarasi na kampuni moja ya kuuza dawa yenye na thamani ya £304m. (Catalunya Radio via Daily Mail)

Mshambuliaji wa zamani wa Celtic Chris Sutton anasema kuwa Pedro Caixinha alikuwa meneja mbaya zaidi wa timu ya Rangers katika historia ya klabu hiyo. (Daily Record)

Image caption Rio Ferdinand

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho ni sharti ashinde mataji baada ya klabu hiyo kuwekeza vikali kulingana na beki wa zamani wa klabu hiyo Rio Ferdinand. (Daily Mail)

Mkufunzi wa Bournemouth Eddie Howe ameelezea droo ya raundi ya tano ya mechi za kombe la Carabao kama mojawapo ya droo kali zaidi.. (Bournemouth Echo)

Mada zinazohusiana