Burnely yaichapa Newcastle 1-0

Burnley haijafungwa katika michezo sita kwenye uwanja wake wa Turf Moor
Image caption Burnley haijafungwa katika michezo sita kwenye uwanja wake wa Turf Moor

Ligi kuu soka England imeendelea usiku wa kuamkia leo kwa mchezo mmoja kupigwa.

Burnley wakiwa nyumbani Turf Moor wameichapa Newcastle United goli moja kwa bila na kufanikiwa kupanda mpaka nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi huku Newcastle ikishuka mpaka nafasi ya tisa.

Goli la Burnley limeweka kimiani na Jeff Hendrick dakika ya 74 ya mchezo.

Newcastle walitawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa hususan kipindi cha kwanza lakini hawakufanikiwa kupata goli.

Baada ya mchezo huo meneja wa Burnley anayehusishwa kujiunga na Everton Sean Dyche amesema kwa sasa hawazi kwenda popote zaidi ya kuifanya Burnley kuwa na matokeo mazuri kwenye ligi kuu EPL.

Burnley imekuwa tishio msimu huu na imeweza kutoa upinzani mkali kwa timu kubwa za ligi kuu ya England.