Kampuni zaidi ya '800,000 nchini Nigeria hazijawahi kulipa kodi'

Nigeria imeanza mikakati mipya na bora ya kuboresha namna ya kukusanya ushuru

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Nigeria imeanza mikakati mipya na bora ya kuboresha namna ya kukusanya ushuru

Zaidi ya makampuni 800,000 nchini Nigeria, yakiwemo yale ya wanakandarasi wa serikali, hayajawahi kulipa kodi. Hayo yamefichuliwa na Waziri wa fedha Kemi Adeosun.

Kupitia taarifa, pia anasema kwamba, ni wanaigeria milioni 14 kati ya milioni sabini wanaochangia uchumi wa taifa hilo kwa njia moja au nyingine, ndio wanaolipa ushuru.

Kati ya watu milioni 14, zaidi ya asilimia 95% wanalipwa mishahara katika sekta isiyo rasmi, lakini watu 241 hupokea mishahara katika sekta ya kibinafsi na ndio ambao walitozwa ushuru iliyofikia dola elfu 65,500 au pauni ya Uingereza elfu 50,000 mwaka 2016, Bi Adeosun amesema.

Kumekuwepo na ukiukaji wa kodi, na sasa serikali imepanga kuchukua kila mbinu ili kuhakikisha kuwa, kodi unakusanywa, aliongeza.

Hii itasaidia kupunguza utegemewaji wa serikali kwa ushuru unaokusanywa pekee kutokana kwa mafuta, Bi Adeosun alimaliza kusema.