Rais Magufuli awasamehe wafungwa 61 wa kunyongwa

Rais Dkt John Magufuli atoa msamaha kwa wafungwa wa kunyongwa na wale maisha.
Image caption Rais Dkt John Magufuli atoa msamaha kwa wafungwa wa kunyongwa na wale maisha.

Rais wa Tanzania John Magufuli kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo amewasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.

Hata hivyo idadi ya wafungwa wengine walioachiwa huru kutokana na makossa mbali mbali ni 1,821 ambao amesema kuwa wanapaswa kuachiwa mara baada ya tangazo lake.

Wafungwa wengine 8157 wamepunguziwa adhabu zao. Idadi hiyo ya msamaha kwa wafungwa inatajwa kuwa ni kubwa katika awamu zote kuwahi kutokea na hasa zinazo wahusisha wafungwa wa kunyongwa na vifungo vya maisha