Beatrice Fihn akabidhiwa tuzo ya Nobel, alaani Nyukilia

Beatrice Fihn akabidhiwa tuzo ya Nobel huko Oslo
Image caption Beatrice Fihn akabidhiwa tuzo ya Nobel huko Oslo

Mshindi wa Nobel Beatrice Fihn na kiongozi wa kampeni ya kimataifa ya kukomesha silaha za Nyuklia amesema dunia ni mahali salama panapo stahili kulindwa na uharibifu dhidi ya silaha za nyukilia.

Fihn ameyasema hayo katika sherehe za kupokea tuzo yake mjini Oslo na pia alikuwa akirejea hali ya sasa kati ya Marekani na Korea Kaskazini kuhusiana na masuala ya nyuklia.

Setsuko Thurlow,manusura wa bomu la atomiki la Hiroshima ambaye ni mshiriki katika tuzo hiyo,dunia inapaswa kupiga vita matumizi ya nyuklia.