Wapiganaji wahukumiwa kufungwa jela maisha kwa ubakaji DRC

Wapiganaji wa Jamhuri ya Congo wahukumiwa maisha kwa ubakaji
Image caption Wapiganaji wa Jamhuri ya Congo wahukumiwa maisha kwa ubakaji

Mahakama ya Mkoa wa Kivu Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewahukumu makumi ya wapiganaji wanaoendesha mapigano nchini humo kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwabaka watoto arobaini akiwemo mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja.

Miongoni mwa waliopatikana na hatia ni kiongozi wa wapiganaji hao pamoja na mbunge mmoja wa eneo hilo.

Awali watuhumiwa hao walidaiwa kufanya vitendo hivyo baada ya kuambiwa na mganga mmoja wa jadi kuwa ingekuwa kinga dhidi ya rasasi kutoka kwa maadui.

Shirika la haki za binadamu linasema hukumu inaashiria kuhitajika kwa jitihada za kukomesha vitendo vya imani zinazosababisha ukatili wa kijinsia.

Kiongozi wa wapiganaji na mbunge wa zamani ni mmoja waliohukumiwa.

Wasichana waliofanyiwa vitendo hivyo watalipwa fidia ya dola 5000.

Mada zinazohusiana