Mkutano wa ECOWAS unafanyika kujadili uchumi siasa na usalama

Wanajeshi wa Senegal Haki miliki ya picha AFP

Viongozi wa mataifa na serikali wa jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi ECOWAS wanakutana leo mjini Abuja nchini Nigeria kujadili changamoto za kiuchumi, siasa na usalama zinazozikabili eneo hilo.

Mkutano huo unafanyika katika wakati ambapo enoe hilo la Afrika magharibi linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mashambulio ya wanamgambo nchini Nigeria, Niger, Mali na Burkina Faso, uharamia katika ghuba ya Guinea na suala la uhamiaji haramu kutoka Afrika kwenda Ulaya.

Ufichuzi wa hivi karibuni kwamba wahamiji wengi wanaotoka Afrika magharibi wanauzwa katika masoko ya watumwa nchini Libya umezusha hasira kimataifa na kumetolewa wito kwa hatua kuchukuliwa kusitisha uhamiaji haramu kuelekea Ulaya.

Baadhi ya wahamiaji, wengi wao kutoka Nigeria, Ghana na Gambians wanalazimishwa kufanya kazi" kama walinzi katika majumba ya kupokea fedha za kikombozi au katika 'soko lenyewe", Mfanyikazi mmoja wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM nchini Niger amesema.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii