Ugiriki inapania kutupilia mbali maombi ya hifadhi ya ukimbizi kwa marubani wa Uturuki

Wanajeshi hao wanasema kuwa hawatapata hukumu iliyo sawa nchini Uturuki Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanajeshi hao wanasema kuwa hawatapata hukumu iliyo sawa nchini Uturuki

Utawala nchini Ugiriki unasema kuwa, umeiomba mamlaka kuu ya mahakama nchini humo, kufutilia mbali uamuzi wa kisheria wa kumpa idhini ya uhamiaji, rubani mmoja wa helikopta, kutoka Uturuki.

Ni mmojawepo wa wanajeshi 8 waliokimbilia Ugiriki, baada ya jaribio la mwaka jana la kumpindua Rais wa Uturuki, Recep Tayyib Erdogan kutibuka.

Uturuki imeonyesha hasira kali, kuhusiana na uamuzi wa kuwapa hifadhi za ukimbizi, huku ukisema utayumbisha kabisa uhusiano wa kidiplomasia wa mataifa hayo mawili.

Wizara ya nchi za kigeni mjini Ankara, inasema kwamba Ugiriki kwa mara nyingine tena umeonyesha, bayana kuwa inawalinda na kuwakumbatia wapangaji wa mapinduzi.

Wanajeshi wengine saba wa Uturuki wamo korokoroni nchini Ugiriki, wakisubiri uamuzi wa maombi yao ya ukimbizi.

Mapema mwezi huu, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu, alizuru Ugiriki na akasema kuwa, hataki kabisa taifa hilo kuwa maficho kwa wapangaji wa mapinduzi.

Zaidi ya watu 250 walifariki na wengine 2,196 wakajeruhiwa pale walipokuwa wakipigana na sehemu moja ya kikosi cha usalama kilichopanga mapinduzi hayo mnamo Juali 15 mwaka jana wa 2016.

Mapinduzi hayo ambayo utawala wa nchi hiyo unasema uliandaliwa nje ya nchi na Muhubiri wa kiislamu, mtoro anayeishi nchini Marekani Muhammed Fethullah G├╝len Hocaefendi, yalitibuliwa

Tangu wakati huo serikali ya Rais Erdogan bado inawasaka watu wanaodhaniwa walishiriki, walipanga au walihusika kwa njia moja au nyingine.

Zaidi ya wafanyikazi wa umma wapatao 150,000 wamefutwa kazi nhuku wengine 50,000 wakikamatwa na kuzuiliwa kortokoroni.

Wapinzani wa Bwana Erdogan, wanasema kuwa hizo ni mnibu zake za kuzima upinzani na wakosoaji wake wa kisiasa.