Mateka 700 wa Boko Haram wafanikiwa kutoroka Nigeria

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram
Image caption Wapiganaji wa kundi la Boko Haram

Jeshi la Nigeria limesema kuwa zaidi ya watu 700 waliokuwa wanashikiliwa na kundi la wapiganaji wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa taifa hilo wamefanikiwa kutoroka.

Msemaji wa jeshi Kanal Timothy Antigha amesema kuwa wamefanikiwa kutoroka kupitia visiwa kadhaa vya ziwa Chad na kufanikiwa kufika katika mji wa Monguno, katika jimbo la Borno.

Hakuna maelezo na ushahidi zaidi kuhusiana na taarifa hizo zilizotolewa na jeshi hilo na mwandishi wa BBC anasema kuwa huenda kutoroka huko kwa watu waliokuwa wakishikiliwa na Boko Haram ni ndani na kipindi kirefu.

Jeshi linasema kuwa operesheni ya hivi karibuni imesdhoofisha nguvu za kundi hilo la Boko Haram. Katika Hotoba yake ya mwisho wa mwaka rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema kuwa kundi hilo limekwisha sambaratishwa.