Nottingham yaitupa nje ya kombe la Fa Arsenal

Nottingham Forest. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nottingham Forest

Bingwa mtetezi wa michuano ya kombe la Fa klabu ya Arsenal imeondolewa katika michuano hiyo kwa kuchapwa 4-0 na Nottingham Forest.

Beki wa Nottingham Forest Eric Joseph Lichaj alifunga magoli mawili katika kipindi cha kwanza beki wa Arsenal Per Mertesacker na Dan Welback wakachomoa magoli hayo.

Penati mbili zilipongwa na Ben Brereton na Kieran Dowell zikawamaliza Arsenal na kuwaondosha mashindanoni.

Katika michezo mingine ya kombe hilo Tottenham walishinda kwa goli 3-0 dhidi ya kalbu ya AFC Wimbledon magoli ya Spurs yalifungwa na Harry Kane aliyefunga magoli mawili na beki Jan Vertonghen akahitimisha kazi kwa goli la tatu.

Newport County wakawatambia Leeds United kwa kuichapa kwa mabao 2 - 1, Shrewsbury Town wakawavuta shati West Ham United kwa sare ya bila kufungana.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii