Watu 6 wauawa katika maandamano DRC

Polisi nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo wakitawanya waandamanaji
Image caption Polisi nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo wakitawanya waandamanaji

Waandamanaji sita wameuawa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo kufuatia makabiliano na polisi waliokuwa wakizima maandamano yanayoendelea kusambaa nchini humo kumshinikiza rais Joseph Kabila kuondoka madarakani, kwa mujibu wa taarifa za Umoja wa Mataifa.

Polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji mjini Kinsasa, ambapo maandamano kama hayo pia yanaendelea katika miji mingine ndani ya taifa hilo.

Msemaji wa umoaja wa mataifa nchini Jamhuri ya Congo amesema kuwa zaidi ya watu 50 walijeruhiwa siku ya Jumapili.

Waziri wa zamani Jean Baptise Sondji ameliambia shirika la habari la AFP kwamba alishuhudia mauaji ya mtoto mwenye umri wa miaka 16 nje ya kanisa eneo la Kitambo mjini Kinsasa.

Serikali ya Congo imepiga marufuku maandamano ya aina yoyote.Siku ya jumamosi mawasiliano ya internet yalikatwa mjini Kinshasa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii