Je Weah ni maarufu kiasi gani nje ya Liberia?
Huwezi kusikiliza tena

Mlinzi matata wa timu ya taifa Kenya, Mickey Weche aelezea umaarufu wa Weah dimbani

Mchezaji nyota wa kandanda wa zamani wa Liberia, George Weah, leo anaapishwa kuwa Rais wa nchi mjini Monrovia pamoja na naibu wake Jewel Howard Taylor.

Weah alivuma sana uwanjani, na miongoni mwa wachezaji aliopambana nao ni mlinzi matata wa timu ya taifa ya Kenya Mickey Weche mwaka wa 1989 katika mechi za kufuzu kwa kombe la dunia.

John Nene amezungumza na Weche atueleze zaidi umaarufu wa Weah uwanjani na jinsi alivyokabiliana naye.