Watu 27 wauawa katika mlipuko Libya

Aftermath of car bomb attack in Libyan city of Benghazi (24 January 2018) Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi na raia walifariki wakati wa shambulio hilo

Takriban watu 27 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa karibu na msikiti mmoja katika mji wa Benghazi nchini Libya utokana na shambulio la kigaidi.

Washambuliaji walitumia gari lenye vilipuzi kutekeleza mpango wao huo.

Milipuko hiyo miwili nje ya msikiti karibu na eneo la Al Suleiman, ilitokea jioni katika swala ya maghari,ambapo waumini hao wakati wanatoka ndani ya msikiti ndipo walipolengwa na shambulio hilo.

Vipande vya picha za video zilizoonyeshwa kupitia televisheni ya taifa,zimeonesha miili ya watu waliouawa katika shambulio hilo ikiwekwa ndani ya gari la Polisi.

Katika shambulizi hilo gari la kwanza lilifika wakati waumini wakitoka na kulipuka,ambapo gari la pili katika shambulizi hilo lililipuka muda mfupi upande wa pili wa mtaa huo dakika chache baadaye lililobeba vilipuzi

Wanajeshi pamoja na raia ni miongoni mwa watu waliathiriwa na shambulizi hilo.

Hata hivyo idadi ya watu waliojeruhiwa na vifo huenda ikapanda kutokana na watu wengi kujeruhiwa.

Bado haijafahamika kwamba ni kundi gani lililoshiriki katika shambulizi, kwani hakuna ujumbe wowote uliotolewa kukiri kushiriki.

Image caption Benghazi eneo linalokumbwa na mashambulizi ya Kigaidi

Mji wa Benghazi umekuwa kitovu cha machafuko kati ya wapiganaji na vikosi vya serikali.

Hata hivyo pamoja na kwamba Libya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya mambomu,lakini milipuko miwili ndani ya dakika 15 ni jambo lisilo la kawaida

Taifa la Libya lilijikuta katika machafuko Zaidi, baada ya kuangushwa kwa utawala wa Muamma Gaddafi mwaka 2011,ambapo makundi yanayotaka kutwaa madaraka yakaibuka na hivyo kutoka mwanya wa kundi la kigaidi la Islamic state kuimariki nchini humo.

Mada zinazohusiana