Watanzania 9 kusimamia mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika

Watanzania 9 kusimamia mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika
Image caption Watanzania 9 kusimamia mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika

Waamuzi nane kutoka Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF kuchezesha mechi za ligi ya Mabingwa Africa na kombe la shirikisho.

Kati yao waamuzi wanne kati yao wameteuliwa kuchezesha mchezo wa ligi ya mabingwa kati ya Lydia Ludic Burundi Academic ya Burundi na Rayon Sports ya Rwanda.

Mwamuzi Mfaume Ali Nassoro atakuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na msaidizi namba moja Frank John Komba, wakati mwamuzi msaidizi namba mbili atakuwa Soud Idd Lila na wa akiba ni Israel Omusingi Njunwa Mujuni huku kamishna wa mechi hiyo akitokea nchini Zimbabwe Gladmore Muzambi.

Mchezo huo utachezwa kati ya Februari 20 na 21, 2018 nchini Burundi.

Waamuzi wengine wanne wa Tanzania watachezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Masters Security Services FC ya Malawi dhidi ya Atletico Petroleos de Luanda ya Angola utakaochezwa kati wa pili kati ya tarege 20 na 21,mwaka nchini Malawi. Fursa kama hizi kwa miaka mingi zimekuwa adimu kwa wataalam wa masuala ya soka kutoka Tanzania na nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.