Uingereza yauza ubalozi wake Thailand

Uingereza
Image caption Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza

Uingereza imenunua ubalozi wake ulioko nchini Thailand kwa zaidi ya dola milioni tano na sitini na saba na inaarifiwa kuwa ni mauzo makubwa kuwahi kutokea kwa mali ama Ofisi zilizoko Nje ya nchi hiyo.Fedha iliyopatikana ni mara tatu ya bajeti ya kila mwaka .

Wafanyakazi kutoka jengo hilo la kikoloni katika mji mkuu, Bangkok watahamishiwa katika sehemu ingine katika jengo lenye mnara .

Fedha zilizo patikana baada ya uuzwaji wa jengo hilo zitatumika kufanyia ukarabati majengo ya balozi zingine za Uingereza ulimwenguni kote.

Mada zinazohusiana