Upandikizaji wa visikizi kwa watoto waliozaliwa na tatizo la usikivu.

Upandikizaji wa visikizi kwa watoto waliozaliwa na tatizo la usikivu.

Nchini Tanzania, kumefanyika muendelezo wa upasuaji na upandikizaji wa vifaa maalumu kwa watoto waliozaliwa na tatizo la usikivu. Upasuaji huo, ni hatua muhimu nchini humo, ambapo wagonjwa hivi sasa wataweza kuipata huduma hiyo bila kusafiri na kupata matibabu hayo kwa gharama kubwa zaidi. BBC umeshuhudia upasuaji huo ukifanyika katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.