ANC chazidisha shinikizo dhidi ya Zuma

Rais Jacob Zuma atakiwa kujiuzuru Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Jacob Zuma atakiwa kujiuzuru

Subira inawaishia viongozi wa chama tawala Afrika kusini ANC dhidi ya rais wa Jacob Zuma waliomtarajia kujiuzulu baada ya majadilianoa ya wiki kadhaa sasa.

Hapo jana usiku viongozi wa chama cha ANC walitangaza kwamba wataitisha mkutano wa kiwango cha juu wa kamati ya kitaifa NEC kuondosha mzozo wa kisiasa kwa lazima.

Mkutano huo unaotarajiwa siku ya Jumatano unatafanyika siku moja kabla ya hotuba ya bunge ya kila mwaka anayotarajiwa kuitoa Zuma bungeni.

Matarajio ni kwamba NEC itapiga kura kumuondoa madarakani.

Lakini Zuma anaweza kwenda kinyume na matakwa ya chama. Hilo basi litaweza kuzusha uwezekano mkubwa na ambao haujawahi kufanyika wa wabunge wa ANC kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

HIzi ni siku muhimu katika demokrasi ya Afrika kusini.

Kauli ya chama cha ANC iliyotolewa kuhusiana na mkutano huo imesema kuwa, wanakutana kujadili ubadilishanaji madaraka kutoka Rais Zuma kama mwenyekiti wa zamani na sasa Cyril Ramaphosa ambaye ni kiongozi mpya wa chama hicho.

Siku ya jumatatu viongozi wandamizi wa chama hicho walilazimika kuwa na mkutano wa dharula mjini Johannesburg kujadili hatima ya rais Zuma.

Hata hivyo rais Zuma ameshikilia msimamo wake kutokubaliana na shinikizo la kumtaka aachie madaraka.

Mwezi Disemba mwaka jana Ramaphosa alimrithi rais Zuma katika nafasi ya juu ya kukiongoza chama hicho kikongwe barani Afrika.

Rais Zuma amekuwaakiandamwa na kashfa za rushwa, ambapo katika miaka ya hivi karibuni alihusishwa na familia yenye asili ya India ijulikanayo kama Gupta - ambapo inadaiwa alitumia madaraka yake vibaya ili kujinufaisha yeye na washirika wake hao.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii