Keoman Mrithi wa Dick Advocate Uholanzi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ronald Koeman amrithi Dick Advocate

Meneja wa zamani wa Everton Ronald Koeman amechaguliwa kuwa meneja wa Timu ya taifa ya Uholanzi, Koeman aliondolewa Everton mwezi Oktoba na amesaini kandarasi ya miaka minne na nusu hadi kufikia mwaka 2022.

Anachukua mikoba ya Dick Advocate ambaye alijiuzulu baada ya kushindwa kuongoza Uholanzi kufuzu fainali za Kombe la Dunia ya 2018.

Koeman amesema anamatarajio mazuri kwa timu yake mpya kwa kuwa Uholanzi ina vipaji vya kutosha lakini watapaswa kubadilisha baadhi ya mambo ambayo atayasema hapo baadaye.