Swansea yaiua Notts County 8-1 FA CUP.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tammy Abraham

Michuano ya FA CUP imepigwa Jana usiku kwa michezo mitatu, Swansea city wakafanikiwa kuwabamiza Notts County kwa kichapo cha mabao 8 -1 , kwa magoli ya Tammy Abraham,Nathan Dyer, Kyle Naughton, Wayne Routledge, Tom Carroll na Daniel James Huku bao la kufutia machozi la Notts County likifungwa na Noor Husin.

Michezo mingine Rock del ikishinda bao 1-0 dhidi ya Mill wall ,Birmingham city ikichakazwa na Hudders field kwa bao 4-1.