Heather Watson na Johanna Konta waanza vizuri

Johanna Konta
Image caption Johanna Konta

kwa kuwashinda wapinzani wao Estonia na kutinga hatua ya nusu fainali.

Heather Watson na Johanna Konta wameshinda mechi zao kwa ushindi wa moja kwa moja katika ushindi wa seti 3 -0.

Wacheza Tenis hao kutoka Uingereza wanataraji kucheza michezo yao wa mwisho na timu ya kundi B siku ya ijumaa na kama watashinda watacheza na washindi wa kundi C.

Mshindi wa mchezo huo atafuzu katika michuano ya Dunia mwezi wa nne Mwaka huu.Michuano hiyo imepangwa katika makundi manne ambayo ni kundi A lenye timu za Serbia,Bulgaria,na Georgia wakati kundi B ni Uingereza,Estonia na Ureno,Kundi C ni Croatia,Hungary na Slovenia na kundi D Latvia,Polanda na Austria.